RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ally Mwinyi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Canada nchini Tanzania, Kyle Nunas, pamoja na ujumbe wa Wenyeviti wa Jumuiya ya Mabunge ya Canada na Afrika, ikiwa ni jitihada za kukuza ushirikiano na kubadilishana mawazo katika masuala ya kiuchumi na kijamii.
Katika mazungumzo yao, Rais Dk Mwinyi amesistiza umuhimu wa sekta ya utalii kwa uchumi wa Zanzibar na kuiarika Canada kutafakari fursa zilizopo katika uchumi wa buluu. Pia kuajidili ushirikiano katika miradi ya huduma za kijamii kama elimu na afya.
Pamoja na hayo yote, Rais Dk. Mwinyi ametumia fursa hiyo kuelezea umuhimu wa Muungano wa Tanzania na kusisitiza masuala muhimu kama uhuru wa habari na uwakilishi wa wanawake katika nafasi za uongozi.
Aidha mkutano huo imekuwa fursa muhimu ya kufungua milango ya ushirikiano na fursa za uwekezaji kati ya Zanzibar, Tanzania, na Canada, huku ukiimarisha mahusiano ya kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili.