Rais Mwinyi aondoa kodi kwenye sukari
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi ameondoa msamaha wa kodi ya ongezeko la thamani(VAT) kwenye bidhaa ya sukari ili kuwasaidia wananchi kuelekea mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kutopanda bei ya bidhaa hiyo.
Rais Dk Mwinyi amesema hayo akizungumza na wafanyabiashara wa Soko kuu la Jumbi na Soko la samaki Malindi Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe:26 Februari 2024 katika ziara yake maalumu ya alipotembelea masoko na kusikiliza changamoto zao.
Aidha,Dk.Mwinyi amewaomba wafanyabiashara kutopandisha bei ya vyakula kiholela bila ya sababu za msingi kwa kupandisha mara mbili ya bei ili kuwasaidia wananchi wanyonge kuelekea mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amewasisitiza Taasisi ya uwezeshaji wananchi kiuchumi Zanzibar(ZEEA) kuwawezesha wafanyabiashara wa soko la samaki Malindi kwa kuwapatia mitaji ili kuendeleza biashara zao.