Rais Mwinyi: Mkitaka kujiuzulu waambieni mabosi zenu

RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi amewataka viongozi wenye nia ya kujiuzulu kueleza sababu za kufanya hivyo kwa kiongozi aliyewateuwa na sio kujichukulia maamuzi binafsi.

Rais Dk Mwinyi amezungumza hayo leo Februari 1, 2024 wakati akiwaapisha mawaziri wateule wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Ikulu ya Zanzibar.

“Sababu nyingine ya waziri kujiuzulu ni pale ambapo serikali inaamua jambo na wewe ukubaliani nalo, unatoka unajiuzulu kwasababu ukubaliani na maamuzi yaliyotolewa na serikali lakini kuna jambo moja lazima tukumbushane wakati unawajibika kwa njia yeyote ile ya kwanza au ya pili ni lazima uwe mkweli na ukweli naozungumzia hapa ni kama kuna mgongano wa maslahi utangaze,”

Advertisement

“Kama tumezuia kitu na wewe una biashara hiyo tangaza, sema ukweli, sema ukweli hapa kuna mgongano wa kimaslahi mimi ni muagizaji wa kitu fulani na ninyi mmezuia, lazima tuwe wa kweli sasa hivi ukitoka halafu ukaenda kuwaamisha watu kinyume chake si sahihi.” Amesema Dk Mwinyi