Rais Samia aadhimisha siku ya kuzaliwa kwa namna hii

ZANZIBAR: Rais Samia Suluhu Hassan ameungana na wananchi wa makundi mbalimbali kupanda miti 4720 inayotarajiwa ikiwemo miti 120 ya matunda.

Miti hiyo imepandwa katika eneo la Donge Muwanda jimbo la Tumbatu lenye ukubwa wa ekari 35.7 ikiwa ni maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ya Rais Samia.

Mkuu huyo wa nchi amesema siku hii inaadhimishwa kwa kupanda miti kwasababu
ya kuwepo kwa uharibifu mkubwa wa mazingira nchini hasa visiwani Zanzibar.

Rais Samia amesema upandaji wa miti kwa wingi pamoja na mikoko kutasaidia
kurudisha hali asilia ya bahari na kupunguza kasi ya mmomonyoko wa ardhi.

Rais Samia ametoa wito kwa wananchi wa eneo hilo kuitunza miti hiyo ili imee na
kuwa na manufaa kwa vizazi vijavyo.

Rais Samia ameitaka Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar kuzuia
uchimbaji wa mchanga kiholela pamoja na kusitisha shughuli za kukata matofali ya
miamba na kutoa vibali vya uchimbaji kwa wananchi wanaokaa maeneo ya juu tu.

Kwa upande mwingine, Rais Samia amezungumza kwa njia ya simu na Mkuu wa
Mkoa wa Njombe Antony Mtaka, na kuwataka viongozi wa mkoa huo
kuendelea kutoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa lishe bora kwa watoto ili
wakue vizuri.

Habari Zifananazo

Back to top button