Rais Samia aagiza kampuni za umma kufanyiwa tathmini

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemuagiza Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu kufanya tathmini kwenye mashirika ya umma ili kubaini mashirika yaliyoshindwa kujiendesha na hivyo kuisababishia serikali hasara.

Rais Samia ametoa agizo hilo leo Juni 17, 2023 kwenye sherehe za miaka 25 ya Benki ya NMB, iliyoambatana na kutoa gawio kwa serikali.

“Serikali imeunda mashirika haya ili yasaidie kupata fedha zitakazosaidia kubeba mzigo wa serikali na si mashirika kula serikalini bila kurudisha faida kwa hiyo msajili nimekupa baraka zote.

” amesema Rais Samia.

Rais Samia amewataka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kujitathmini namna na utendaji kazi wao “kajitizame vizuri ndani ya shirika, wengine wote kajitizameni vizuri hii haina kurudi nyuma, kuna nitakayofuta, nitakayosaidia na nitakayoipa miongozo jinsi ya kujiendesha ili wote mfanye faida.

“Nasubiri taarifa ya mwisho ya mashirika gani yanabaki na yapi yanaondoka na yapi yasaidiwe vipi kufanya biashara, na siku tutakapoyatangaza wale ambao tutatoa fedha mfukoni kuyapa na kuyasaidia nitawaambia siku mashrika hayo yakifa wafe nayo, sitaki kuona shirika linazorota afu meneja anavaa suti nzuri mtaani, hatutaenda pamoja.” Aliongeza Rais Samia.

Habari Zifananazo

Back to top button