Rais Samia achangia Sh Mil 500 timu za Taifa

DAR ES SALAAM: RAIS Samia Suluhu Hassan na rafiki zake amezichangia timu za Taifa Sh milioni 500.

Pia msanii wa Bongo Fleva Ally Saleh maarufu Ally Kiba amezichangia timu hizo Sh milioni 20.

Harambee hiyo iliyofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Johari Rotana jijini Dar es Salaam, imeongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambae alisema lengo ni kukusanya Sh bilioni 10 ambazo zitagawanywa kwa timu zote za Taifa.

Aidha, Rais Samia akipiga simu kuchangia harambee hiyo alisema “michezo ni jukumu letu, jukumu la serikali, jukumu la watanzania, serikali tumejitahidi sana kukuza michezo, serikali tumetoa vivutio timu zimetuitikia, ” amesema na kuongeza

” Lakini tumefika mahali tuna uchache wa bajeti, nawaomba tuchangie ili timu zetu ziende kushindana na sio kushiriki, kwa kuanzia mimi na rafiki zangu tutatoa Sh milioni 500,” amesema.

Habari Zifananazo

Back to top button