Rais Samia afanya kikao maalum na Mwigulu

SIKU moja baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kufanya mkutano cha wazi na wafanyabiashara wa Kariakoo, Rais Samia Suluhu Hassan  amekutana  na watendaji mbali mbali wa Wizara ya Fedha wakiongozwa na Waziri wa Wizara hiyo Mwigulu Nchemba.
Kikao hicho maalum, kimefanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo Mei 18,2023 kikiwakutanisha pia  Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara wakiongozwa na Waziri wake Dkt. Ashatu Kijaji, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakiongozwa na Kamishna Mkuu Alphayo Kidata pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Moses Kusiluka.
Kikao hicho maalum kimekuja ikiwa ni siku moja baada ya Waziri Mkuu kufanikiwa kuzima mgomo wa wafanyabiashara wa Kariakoo ambao wakilalamikia utitiri wa Kodi.
/* */