Rais Samia afanya mabadiliko baraza la Mawaziri

Angellah Kairuki ndani, Bashungwa Waziri wa Ulinzi

RAIS Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri leo Septemba 2,2022
Katika uteuzi huo, Rais  Samia amemteua Dkt. Stergomena Lawrence Tax kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
 Awali Dkt.Tax alikuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Dk Tax anachukua nafasi ya  Balozi Liberata Mulamula.
Pia,  amemteua  Innocent  Bashungwa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Kabla ya uteuzi huo Bashungwa alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Pia Rais Samia amemteua  Angellah Kairuki kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha, amemteua pia  kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Kurugenzi Mawasiliano Ikulu, mawaziri wote walioteuliwa wataapishwa  kesho Oktoba 3, 2022 saa 3:00 asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button