Rais Samia afanya mabadiliko Wakuu wa Mikoa

Mtanda, Kihongosi waula

RAIS Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Wakuu wa Mikoa huku akitemteua Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Kenani Kihongosi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Urambo.
 
Kihongosi anachukua nafasi ya Said Mtanda ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
 
Mtanda amechukua nafasi ya Meja Jenerali Suleiman Mungiya Mzee ambaye atapangiwa majukumu mengine.
 
Katika taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Zuhura Yunus iliyotolewa leo Mei 23, 2023 Rais Samia pia amemuhamisha Queen Sendiga kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara akichukua nafasi ya Makongoro Nyerere ambaye amehamishwa kwenda Rukwa.

Habari Zifananazo

Back to top button