Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko katika safu ya wakuu wa wilaya leo Julai 2, 2023.
Rais Samia ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mwanahamisi Munkunda na kumteua Mobhare Holmes Matinyi kuwa mkuu wa Wilaya ya Temeke.
Ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Abel Yeji Busalama amemhamisha kituo Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Hashim Shaib Mgandilwa kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilindi.
Amemteua James Wilbert kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mjini
Taarifa hiyo imetolewa na na kurugenzi ya mawasiliano ikulu na kusainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Zuhura Yunus.
Comments are closed.