Rais Samia afanya uteuzi makatibu, manaibu

RAIS Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa makatibu na manaibu katibu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI ) na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).

Taarifa iliyotolewa leo Juni 13, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Zuhura Yunus amesema, Rais Samia amemteua Mhandisi, Rogatus Mativila kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Tamisemi (miundombinu).
Mativila alikuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).

Pia, amemteua Mhandisi Mohamed Besta kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).
Besta ni Mkurugenzi wa Ufundi wa Wakala wa Usimamizi wa Usalama wa Usafiri wa Anga wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (CASSOA) akichukua nafasi ya Mativila ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu.

Rais Samia pia, amemteua Kamishna Benedict Wakulyamba kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii.

Kamishna Wakulyamba anachukua nafasi ya Anderson Mutatembwa ambaye amehamishiwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu

Amemteua Mhandisi Amin Mcharo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button