RAIS Samia Suluhu amemteu Anamringi Macha kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, kabla ya uteuzi huo Macha alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Zuhura Yunus imeeleza kuwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais ( Muungano na Mazingira).
Aidha, Rais Samia amemteua Japahari Kubecha Mghamba kuwa Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, kabla ya uteuzi huo, Mghamba alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Busega.
Aliyekuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kaliua, Mussa Kilakala ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Pangani.