Rais Samia afanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi, Msajili

RAIS Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali akiwemo Mhandisi Othman Sharif Khatib ambaye anakwenda kuwa mwenyekiti wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Mhadisi Khatib anachukua nafasi ya Dk Jones Kilembe ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Rais Samia pia amemteua Bw. Sosthenes Laurent Kewe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Maendeleo ya Tanzania (TIB). Kewe anatoka Sekta Binafsi akiwa ni Mshauri Binafsi wa Uendelezaji wa Sekta Binafsi za Fedha jijini Dar es Salaam.

Vilevile, Rais Samia amemteua Dk David Nkanda Manyanza kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI). Dk Manyanza ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Development Solution Consultancy (T) Limited.

Wakati huo huo, Rais Samia amemteua Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Morogoro Bw. Sylvester Joseph Kainda kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani.

Taarifa ya Ikulu imesema uteuzi huo unaanza mara moja.

Habari Zifananazo

Back to top button