Rais Samia aialika Yanga Ikulu

RAIS Samia Suluhu Hassan kesho Juni 05, 2023 ameialika timu ya Yanga kupata chakula cha jioni Ikulu, Dar es Salaam ikiwa ni pongezi kwa kufanya vizuri katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa ametoa taarifa hiyo leo, ambapo amesema Rais Samia amewapongeza Yanga kwa kucheza vizuri katika mchezo fainali ya pili hapo jana na kuwafunga USM Alger bao 1-0.

Ushindi huo ulifanya matokeo ya jumla kusomeka 2-2 hata hivyo Yanga ilipoteza nafasi ya ubingwa kutokana na kanuni ya FIFA namba 55 ya goli la ugenini, ambapo Yanga iliruhusu mabao mengi (2) ikiwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Msigwa amebainisha kuwa pamoja na kutotwaa ubingwa, Rais Samia anatambua kuwa Yanga wameipa heshima kubwa Tanzania na anawapongeza wachezaji na benchi la ufundi na viongozi wa timu hiyo.

Kwa kumaliza nafasi ya pili, Yanga imetwaa Dola milioni 1 ambazo ni sawa na Sh bilioni 2.3. Bingwa USM Alger ametwa Dola milioni 2 ambazo sawa na Sh bilioni 4.7

Timu ya Yanga, viongozi na mashabiki wanatarajiwa kurejea leo kwa ndege iliyotolewa na Rais Samia ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono timu hiyo iliyokuwa ikiiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x