Rais Samia aingilia kati mgogoro wa Yanga, Fei Toto

Aitaka Yanga imalizane na Fei

RAIS Samia Suluhu Hassan ameitaka Klabu ya Yanga kumaliza mgogoro na kiungo Feisal Salum ‘ Fei Toto’.

Rais Samia ametoa agizo hilo leo June 5, 2023 katika hafla ya chakula ya jioni ya kuwapongeza Yanga kwa kushiriki fainali za michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika juzi Juni 3,2023 dhidi ya US Alger ya Algeria.
Akizungumza Rais Samia amesema “sifurahi migogoro kati ya viongozi na wachezaji, issue ya Fei Toto mkaimalize.

“Haipendezi klabu kubwa kama hii kuwa na ugomvi na mtoto mdogo,  hebu kamalizeni,  kisha mje nyumbani kunieleza.

” Amesema

Yanga wamekuwa na mgogoro wa kimkataba wa muda mrefu na kiungo huyo humu Kamati ya Sheria na Hadhi ya wachezaji ambayo ilisikiliza malalamiko ya pande zote na kuamua kuwa mchezaji huyo bado anamkataba na Yanga mpaka 2024.
Fei aliondoka Yanga kuanzia mwishoni mwa mwaka jana, baada ya kudai kuwa anahitaji maslahi zaidi, akavunja mkataba kwa kuweka kiasi cha Sh milioni 112 kwenye akaunti ya klabu hiyo, lakini baadaye Kamati ya Sheria Hadhi za Wachezaji iliyopo chini ya Shirikisho la Soka Tanzania TFF, ilisema kuwa mchezaji huyo bado ni mali ya Yanga kwa kuwa hakufuata taratibu za kuvunja mkataba huo.

Habari Zifananazo

Back to top button