Rais Samia alia na nidhamu jeshi la polisi

DAR ES SALAAM: Rais Samia Suluhu Hassan ameeleza kusikitishwa na tabia ya utovu wa nidhamu kwa baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi na kumtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali wa Polisi (IJP) ‘kukaza buti’ Jeshi linyooke.

Akizungumza wakati wa Hafla ya ufunguzi wa Kikao Kazi cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo, Rais Samia amesema inasikitisha kuona bado kuna tatizo la nidhamu katika jeshi la polisi.

“Kuna kesi tunapokea, zingine tunaona katika mitandao mtu akipotoka.

Bado kazi ipo ila nikiri kuwa kidogo kidogo mabadiliko yataendelea kuwepo kutokana na mafunzo wanayoyapata,” amesema Rais Samia. Imeandaliwa na Mwandishi Wetu

Habari Zifananazo

Back to top button