ZANZIBAR: RAIS Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Said Othman Yakub kuwa Balozi wa Tanzania nchini Comoro.
Balozi Yakub anachukuwa nafasi ya Balozi Pereira Ame Silima aliyemaliza muda wake.
Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Zuhuru Yunus imeeleza kuwa uteuzi huo unaanza mara moja.