Rais Samia amuapisha Dk Mataragio

ZANZIBAR: Rais Samia Suluhu Hassan amemuapisha Dk James Peter Mataragio kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Ndogo Tunguu, Zanzibar leo Machi 5, 2024.

Mataragio aliteuliwa Februari 21,2024 akichukua nafasi ya Athuman Mbuttuka ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na atapangiwa kazi nyingine.

Dk Mataragio ameapa leo baada ya  mwaka mmoja kuwa nje ya nafasi za uteuzi, tangu alipotenguliwa katika wadhifa wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Februari 24, 2023.

Safari ya Dk Mataragio katika nafasi za uteuzi nim ilima na mabonde akiwa Mkurugenzi wa TPDC, aliwahi kutenguliwa na saa chache baadaye akateuliwa tena kurudishwa kwenye wadhifa huo.

Hayo yalitokea usiku wa Aprili 4, 2021, Rais Samia alipoamua kutengua uteuzi wa Dk Mataragio ndani ya TPDC na kesho yake asubuhi, Aprili 25 alimteua kurudi kwenye nafasi hiyo aliyodumu nayo hadi Februari 24,2023 alipotenguliwa tena.

Habari Zifananazo

Back to top button