Rais Samia anogesha Prof Jay Foundation kwa Sh Mil 50

DAR ES SALAAM: Rais Samia Suluhu Hassan amechangia kiasi cha Sh milioni 50 kwa Taasisi ya Profesa Jay Foundation iliyochini ya msanii, Joseph Haule maarufu Prof Jay inayosaidia wagonjwa wa figo.

Pia amesema kuwa endapo itafikia hatua ya kutaka kumpandikiza Profesa Jay figo atatoa gharama za matibabu hayo yenye thamani ya Sh million 47.

Aidha Rais Samia ameitaka Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Mkurugenzi mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa Mohamed Janabi kuandaa mpango mzuri wa Profesa Jay kuendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Taasisi hiyo ya Prof Jay Foundation imezinduliwa rasmi usiku wa kuamkia Desemba 11, 2023 jijini Dar es Salaam.

Habari Zifananazo

Back to top button