Rais Samia aonya mabalozi kutoingilia uchaguzi

DAR ES SALAAM: Rais Samia Suluhu Hassan amewaonya mabalozi kuacha kuingilia uchaguzi na badala yake waheshimu miiko ya diplomasia.

Rais Samia ameyasema hayo katika sherehe za mwaka mpya 2024 kwa mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini pamoja na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa zilizofanyika Ikulu.

“Serikali itaendeza ushirikiano na balozi zote kwa mujibu wa katiba, tunu za kitaifa, usawa, umoja na mshikamano wa kitaifa….; “Msiingilie uchaguzi wetu, kuzingatia mila, kanuni na maadili ya diplomasia.” Amesema

Rais Samia ametoa kauli hiyo ikiwa ni miezi michache kukaririwa akisema kuwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024, utoe taswira ya uchaguzi utakaofuata wa mwaka 2025.

Ametaka kudumishwa kwa amani na mshikamano miongoni mwa wananchi katika uchaguzi huo, ili kujenga taswira njema ya uchaguzi Mkuu wa 2025.

Wakati huo huo, Rais Samia amesema Tanzania inasikitishwa na vita ya vinavyoendelea Palestina na kusababisha mauaji ya watoto na raia wasio na hatia na inaunga mkono usuluhishi kati ya Palestina na Israel kwa kutoa wito wa kusitishwa mapigano na kuptiwa misaada ya kibinadamu.

Habari Zifananazo

Back to top button