Rais Samia apiga marufuku Wizara kuchukua mapato ya Mashirika

ARUSHA: RAIS Samia Suluhu Hassan amepiga marufuku tabia ya baadhi ya Mawaziri na watendaji wa Wizara kugeuza Mashirika ya Umma kama vyanzo vyao vya mapato akisisitiza mpango huo umekuwa ukidhoofisha mashirika kuchangia katika mfuko mkuu wa serikali.

Akifungua Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma jijini Arusha, Rais Samia amesema kumekuwa na baadhi ya Wizara ambazo zimekuwa zikoomba michango kutoka katika taasisi zilizo chini ya Wizara zao kipindi zinapoishiwa bajeti ya matumizi mengineyo (OC).

“Wizara nyingi zimefanya mashirika kuwa vyanzo vya mapato. Mashirika yanapaswa kuchangia gawio … Wizara zinaweka mikono katika mapato ya mashirika hii haitakiwi kama tunataka mashirika yazalishe tusiyaingilie,” amesema Rais Samia jijini Arusha.

Kwa mujibu wa Rais Samia kuna mashirika yaliundwa kujitegemea lakini yameshindwa kujitegemea na leo ni tegemezi serikalini na pia hayazalishi vizuri.

Rais Samia amesema Serikali imeshatoa pesa nyingi na sasa haiwezi kuendelea kutoa pesa kwa taasisi ambazo hazizalishi. 

Amewatahadharisha Wenyeviti wa Bodi kuwa hatasita kuwafikisha katika mamlaka za sheria wenyeviti wanaoshindwa kuwajibika huku akieleza kuwa Wakuu wa Taasisi zitakazoshindwa kufanya vyema pia wataondolewa.

Taasisi za Umma zimechangia zaidi ya Sh trilioni 1 katika mfuko mkuu wa serikali na Rais Samia anaamini Taasisi hizo zinaweza kuchangia zaidi.

Habari Zifananazo

8 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button