Rais Samia apigia chapuo Kiswahili

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akihutubia Wanachama wa Chama cha Siasa cha Mozambican Liberation Front (FRELIMO) pamoja na viongozi mbalimbali walioalikwa kushiriki Kongamano la 12 la Chama hicho Tawala, Maputo nchini Msumbiji

NCHI za Afrika hususani Msumbiji zimetakiwa kutumia lugha ya Kiswahili kwa kuwa ndio lugha pekee ambayo inaweza kuwaunganisha Waafrika.

Hayo yamesemwa leo Septemba 23, 2022 na Rais Samia Suluhu katika Kongamano la 12 la Chama cha FRELIMO Maputo nchini Msumbiji.

Akizungumza katika Kongamano hilo, Rais Samia amesema baada ya nchi za kusini mwa Afrika kupata uhuru kutoka kwa wakoloni, hazikufanya jitahada za dhati za kukitumia Kiswahili kwa ajili ya kuwaunganisha, lugha ambayo ni muhimu, hivyo  iliyopaswa kutumiwa na nchi hizo baada ya kupata uhuru lakini kwa bahati mbaya zimeendelea kutumia lugha za kigeni.

Advertisement

“Tanzania tunamshukuru Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, kwa kuikuza Lugha ya Kiswahili na kuifanya Tanzania kuwa na lugha moja juu ya makabila yote. Kwa hiyo Kiswahili kinaweza kutumika kama chombo cha kutuunganisha waafrika na ulimwengu,”amesema Rais Samia na kuongeza.

”Nimefurahi kuona wapigania uhuru hapa wakiongea lugha ya Kiswahili, lugha iliyotumika katika harakati za ukombozi, Kiswahili kinaweza kuwa lugha ya kuwaunganisha wananchi wa Msumbiji, comrade Nyusi ona namna kuweka lugha ya Kiswahili katika mfumo wenu wa elimu.”Alisisitiza

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *