Rais Samia apokea Sh bilioni 2 za Hanang

IKULU, Dodoma: Rais Samia Suluhu Hassan amesema maisha ya watanzania walioathirika na maafa ya mafuriko na maporomoko ya tope huko wilayani Hanang mkoani Manyara yatarejea katika hali ya kawaida akiwataka wananchi na mashirika kuendelea kuchangia juhudi za kurejesha huduma katika mji huo.

 

Akizungumza baada ya kupokea hundi ya Sh bilioni 2.1 ikiwa ni mchango wa mashirika ya umma 270 kusaidia waathirika wa maafa hayo, Rais Samia amesema hakuna kitakachozuia kurejeshe maisha ya kawaida kwa walioathirika na maafa hayo.

Mchango huo umekabidhiwa leo, Ikulu mjini Dodoma na Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu kwa niaba ya Mashirika ya Umma kusaidia waathirika wa maafa ya Hanang.

 

“Na huu ndio umuhimu wa kuwa na Mashirika ya umma. Mashirika ya umma lazima yaguswe na yanayotokea kwa umma,” amesema Rais Samia.

 

Amesema amefarijika kwa namna Mashirika ya umma 270 yalivyojitokeza kuchangia kwa viwango tofauti, kwa hiyari yao. Ishara inayoonesha mageuzi katika utendaji wa Mashirika umma.

Pia, Mkuu huyo wa nchi amewashukuru watanzania wote, taasisi, mashirika ya umma na binafsi sambamba na wafanyabiashara kwa kushirikiana kwa pamoja katika kuwasaidia waathirika wa Hanang.

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button