Rais Samia aridhia kufutwa tozo miamala ya simu

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amekubali ombi la Wizara ya Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kufuta tozo za miamala ya simu.

Akizungumza katika ziara yake mkoani Rukwa leo Julai 4, 2023 Naibu Waziri Wizara hiyo, Kundo Mathew amesema hatua hiyo ni faharii na inaonesha namna Rais Samia anavyowasikiliza Watanzania.

“Rais wenu kipenzi mkuu wa nchi ameruhusu na kutoa maelekezo tozo inayotokana na miamala ya simu iondolewe, hakutokuwa na tozo kwenye miamala ya simu, ile tozo mliokuwa mnasema Rais ameshapangua huyu ndio mwanamapinduzi halisi wa maendeleo ya taifa letu.”amesema Naibu Waziri Kundo Mathew.

Advertisement

Naibu Waziri huyo amesema ombi la kufutwa kwa tozo za miamala ya simu liliwasilishwa na Waziri wa Wizara hiyo, Nape Nnauye na baadaye Rais Samia alimjibu Waziri Nape kuhusu kuridhia ombi hilo.

“Hayo ni maelekezo ambayo, Mh Rais ameyatoa kwa Mh Nape Moses Nnauye na mimi msaidizi nitaendelea kuwajulisheni kila ninapopita.”amesema Kundo

1 comments

Comments are closed.