JAJI Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Hamis Juma, amesema uteuzi wa majaji 22 wa Mahakama Kuu uliofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan, unaenda kushusha mzigo wa majaji kutoka wastani wa mashauri 340 hadi 265 kwa mwaka.
Profesa Juma amesema tangu Rais Samia aingie madarakani ameteua jumla ya majaji 52.
Amesema katika kipindi cha miezi 15, Rais Samia ameteua Majaji 9 wa Mahakama ya Rufani na Majaji 43 wa Mahakama Kuu.
Amesema hiyo pia imeongeza uwiano wa majaji wanawake kutoa wastani wa asilimia 35 hadi 38, baada ya idadi ya majaji hao wa Mahakama Kuu kufikia 27 kati ya 78, amesema Prof. Juma
“Tunashukuru kwa kuzingatia uwiano wa kijinsia. Kwa mhimili wa mahakama kupata majaji hawa wote tunaamini huu ni uwezeshaji mkubwa sana,” amesema Jaji Mkuu akiongeza kuwa: “itasaidia kusogeza huduma za haki karibu na wananchi.”