Rais Samia ataka mvuvi wa Precision Air apewe kazi

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa na Majaliwa Jackson

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu ameagiza kijana Majaliwa Jackson, mvuvi aliyeshiriki kuokoa abiria kwenye ajali ya ndege mkoani Kagera akabidhiwe kwa Waziri wa mambo ya ndani na atafutiwe nafasi kwenye jeshi la uokozi ili apate mafunzo ya ujasiri.

Akizungumza katika tukio la kuaga miili ya watu 19 katika Uwanja wa Kaitaba, Waziri Majaliwa amesema Rais Samia alipiga simu akiwa katika viwanja hivyo na kutoa maagizo hayo baada ya kuona ujasiri aliouonyesha kijana huyo.

“Na mimi kama mtendaji mkuu naendelea kumsisitiza waziri wa mambo ya ndani baada ya tukio hili akutane na kijana achukue, anuani zake na kuenda kwenye jeshi la uokozi mara moja, nimhakikishe Mh Rais maagizo hayo tutayasimamie kwa ukaribu,” Majaliwa.

Advertisement

/* */