Rais Samia ataka Somanga wawe na subira

LINDI; Kilwa. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewashauri wananchi wa Somanga Kusini wilayani Kilwa mkoani Lindi kuwa na subira ya miezi 18 hadi 20, ili kuondokana na changamoto ya nishati ya umeme na huduma ya maji.

Rais Samia ameyasema hayo leo alipozungumza na wananchi hao na kusema pia changamoto za wafugaji na masuala ya ardhi serikali itafanyia  kazi.

Rais Samia amesema kwamba serikali itashughulikia suala la maji kwa vijiji 50 kupata huduma ya maji wilayani humo

Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kaskazini, Francis Ndulane aliishukuru serikali kwa kutekeleza miradi ya maendeleo kwenye sekta za afya, barabara na maji.

 

Habari Zifananazo

Back to top button