Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza siku tano za maombolezo na bendera zitapepea nusu mlingoti kuanzia leo Februari 10, 2024 kufuatia kifo cha Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa.
Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango ametoa tangazo hilo katika taarifa yake kwenda kwa umma ya kifo cha kiongozi huyo.
Edward Lowassa amefariki dunia leo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete, Dar es Salaam.
Mwaka 2015 aliwania urais kwenye uchaguzi mkuu akiwa mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambapo John Magufuli aliibuka mshindi wa kiti hicho.