Rais Samia ateua naibu katibu mkuu wizara ya nishati

RAIS Samia Suluhu Hassan amemteua Dk James Peter Mataragio kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati.

Taarifa hiyo imetolewa leo Februari 21, 2024 na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Zuhura Yunus.

Dk Mataragio anachukuwa nafasi ya Athumani Selemani Mbuttuka ambaye uteuzi wake umetenguliwa na atapangiwa kazi nyingine, kwa mujibu wa taarifa hiyo.

Advertisement

Kiongozi huyo aliwahi kuwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC).