Rais Samia atoa maagizo 6 kuepusha migogoro
RAIS Samia Suluhu Hassan ametoa maelekezo sita kwa mihimili ya sheria nchini ili iweze kutoa haki kwa wakati na kuepusha migogoro.
Akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria nchini, yaliyofanyika kwenye viwanja vya Chinangali mjini Dodoma, leo Februari Mosi, 2023, Rais Samia kwanza ametaka marekebisho katika mfumo wa utoaji haki .
“Mfumo wa utoaji haki unaochukua muda mrefu kutatua migogoro ni hatari kwa nchi yetu, uongeza gharama na kuathirika mazingira ya uwekezaji na biashara, laizma turekebishe.”Amesema
Pia, ameagiza mihimili hiyo ya mahakama kuendelea kuweka nguvu katika tafiti za kuleta ufanisi katika utoaji haki na kutumia tafiti hizo kujiwekea mikakati muda mfupi, wa kati na mrefu kuendana na matarajio ya wananchi.
Rais Samia, ameagiza pia kuchukua hatua kwa watumishi wanaochafua sura ya mahakama kwa vitendo vya rushwa, kauli mbaya na vitendo vya udhalilishaji, kwa wanawake, watoto na wenye uhitaji maalum.
“Watendeeni watu vile ambavyo sisi tungependa kutendewa.”Amesema
Aidha, ameagiza kutuzwa kwa miundombinu ya majengo, Tehama ili vitumiwe na vizazi vijavyo na kutaka vitendea kazi vya kisasa viendane na haki kwa wananchi.
“Isiwe tunaimba kuna haki wakati huko nje kwa wananchi hakuna, haki ionekane na ipatikana kwa wananchi.”Amesema Rais Samia
Rais Samia amesema pia anaunga mkono maazimio yote yatakayosaidia kuondoka migogoro ya haki lakini pia malengo yote yatakayogusa nyanja zote kiuchumi, kijami na kisiasa na kwamba yupo tayari kuunga mkono yanayohitaji kuhamasiha ili kufikia lengo.