RAIS Samia Suluhu Hassan, ametoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki kufuatiwa ajali ya basi iliyouwa watu 15 katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtama mkoani Lindi jana.
Ajali hiyo ilitokea mchana ikihusisha basi la Baraka lilipokuwa likitokea Tandahimba kuelekea Dar es Salaam.
Taarifa iliyochapishwa na Rais Samia kupitia mitandao yake ya kijamii imevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuongeza usimamizi wa sheria na ukaguzi.
“Tunapoelekea msimu wa mwisho wa mwaka naviagiza vyombo vyote vya ulinzi na usalama barabarani kuongeza usimamizi wa sheria na ukaguzi.” Amendika.