Rais Samia atoa pole kifo cha Baasaleh

RAIS Samia Suluhu Hassan ametoa pole kwa waumini wa dini ya Kiislamu, kufuatia kifo cha mwanazuoni Sheikh Ali Baasaleh

“Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Sheikh Ali Basaleh, mwanazuoni na mwalimu katika imani,”

“Natoa pole kwa waumini wa dini ya kiislamu, familia, ndugu, jamaa na marafdiki. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amina.” Ameandika Rais Samia kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter.

Advertisement

Sheikh Baasaleh amefariki  Julai 30, 2023 katika hospitali ya Aga Khan, jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

Mwili wa mwanazuoni huyo unatarajiwa kuswaliwa katika msikiti wa Mtoro, Kariakoo na kuzikwa leo Julai 31, 2023 katika makaburi ya Kisutu, Upanga Dar es Salaam.

Enzi za uhai wake sheikh Baasaleh aliwahi kuwa Imamu wa Masjid Idrisa uliuopo Kariakoo, jijini.

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *