Rais Samia atoa pole maafa ya mgodi Shinyanga
RAIS Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita kufuatia maafa yaliyotokea katika Mgodi uliopo wilaya ya Shinyanga Vijijni.
Katika taarifa yake Rais Samia amesema: “Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya maafa yaliyotokea katika Mgodi wa Nyandolwa, Kata ya Mwenge mkoani Shinyanga ambapo ndugu zetu 25 wanaofanya shughuli katika mgodi huo walifukiwa na kifusi.
Nimeielekeza Ofisi ya Waziri Mkuu na vyombo vya ulinzi na usalama kupeleka misaada ya haraka na kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ili kuharakisha zoezi uokoaji ambalo linaendelea.
Tuendelee kumwomba Mwenyezi Mungu awajalie pona ya haraka majeruhi, na pia awape subra na nguvu ndugu, jamaa na marafiki wa wale wote walioathiriwa na maafa haya.”



