Rais Samia atoa Sh milioni 10 kwa wavuvi waliofanya uokoaji
Shughuli uwanja wa Kagera zarejea

RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hassani, ametoa shilingi Milioni 10 kwa wavuvi wa Mwalo wa Nyamukazi ambao walishiriki kufanya uokoaji wa abria katika ajali ya ndege ya Precision iliyotokea Novemba 6 mwaka huu na abiria 19 kupoteza maisha
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Albert Chalamila na maofisa mbalimbali kutoka ofisi ya Waziri Mkuu walifika katika Mwalo wa Nyamukazi na kukutana na wavuvi ambao wameomba kujipangia matumizi juu ya fedha hizo.
Chalamila amemtaka kufunguliwa akaunti maalum ya kuweka fedha hizo ili wavuvi walioshiriki kufanya uokoaji waweze kupanga mikakati ya namna watakavyotumia fedha hizo na namna zitakavyowasaidia .
Hata hivyo shughuli katika uwanja wa ndege wa Bukoba zimerejea kama awali hivyo ratiba ya ndege kutoka katika makampuni mbalimbali kutua na kuondoka inaendelea.