Rais Samia atua Arusha

Atoa matumaini kwa vijana

RAIS Samia Suluhu Hassan ametua mkoani Arusha na kuahidi kufungua njia katika kupunguza tatizo la ajira kwa vijana nchini.

Amesema, serikali yake bado inaangaika kutafuta njia ya kufungua nchi kwa kukaribisha sekta binafsi kufanya nao kazi  katika maeneo tofauti tofauti ili kuongeza ajira kwa vijana.

Rais Samia ameyasema hayo Tengeru mkoani Arusha leo Juni 24, 2023 aliposimama kusalimiana na wananchi wa eneo hilo akielekea Arusha mjini ambako kesho atafunga kilele cha maadhimisho ya dawa za kulevya, katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

“Najua vijana wangu machinga, bodaboda bado kuna mambo ambayo tunapaswa kufanya, lakini mengine yote elimu, afya,umeme tunajitaidi.”Amesema huku akishangiliwa kwa nguvu

“Ahadi ya soko la Tengeru bado haijatizwa nawaaidi ahadi ipo pale pale tunatafuta fedha tuje tuwatimizie.

Aidha, amesema vijana wa vyuo ataendelea kuboresha bajeti ya sekta ya elimu.

“Vijana wa vyuo, bajeti mmeiona, tutaendelea kuboresha, tunasema tuna ‘build better tomorrow’ kwa ajili ya vijana , kwa hiyo wale mliopo kwenye sekta ya kilimo, mifugo, uvuvi na biashara wote tunajipanga vizuri kutoa huduma

“Tunataka kuona vijana wa Tanzania wakiwa wako-busy na kuzalisha mali na kujenga ustawi wa maisha yao na kujijengea uchumi wenye hadhi, uchumi imara kwenye familia zao na taifa kwa ujumla.”Amesema

 

Habari Zifananazo

5 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button