RAIS Samia Suluhu Hassan leo Desemba 28, 2023, ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu ya Usimamizi wa Utalii na Masoko katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Tunguu Zanzibar.
Chuo hicho kimemtunuku Shahada hiyo kwa kutambua mchango wake wa kuifungua nchi kiuchumi kupitia sekta ya utalii.
Rais Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine akiwa kwenye maandamano ya kitaaluma wakati walipokuwa wakiingia kwenye Ukumbi wa Dk Ali Mohamed Shein Kampasi ya Tunguu kwa ajili ya kushiriki Hafla ya Mahafali ya 19 ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA)