Rais Samia Suluhu Hassan ameitaka dunia itambue kuwa Afrika si salama kwa wala rushwa na si kichaka cha ufichaji wa fedha zinazotokana rushwa hiyo
Lakini pia Tanzania imefanya vema katika masuala ya rushwa Afrika huku nchi za China na Singapore zikiwa zimefanya vema zaidi kwenye mapambano hayo na kusisita wataalam wa masuala ya rushwa nchini Tanzania kwenda kujifunza zaidi mapambano hayo.
Rais Samia amesema hayo leo jijini Arusha wakati wa kufunga mkutano wa siku tatu wa Maadhimisho ya Siku ya Kupambana na Rushwa Afrika na maadhimisho ya miaka 20 ya Utekelezaji wa Mkataba wa Kupambana na Rushwa Afrika ikiwemo safari ya Tanzania katika mapambano hayo.
“Nchi zetu si kichaka cha kuficha fedha za wala rushwa na si salama kwa wala rushwa na nataka wala rushwa wajue kuwa hatua zaidi zichukuliwe kwa vitendo kwa wale wote wanaohusika na rushwa.” Amesema Rais Samia.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Masuala ya Rushwa Barani Afrika (AUABC),Pascoal Joaqium amesisitiza kuwa umoja wa Afrika wa Kupambana na Rushwa (AUABC)umeweza kupambana na Rushwa na nchi 15 wanachama ziliwasilisha ripoti zao za Kuzuia na Kupambana na Rushwa ambapo nchi 11 ziliwasilisha ripoti zao huku Tanzania ikiwa ni mojawapo ya nchi iliyowasilisha ripoti hiyo.