Rais Samia awateua, Diamond, Shilole

Rais wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan amemteua mwimbaji wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul Diamond Platnumz na mjasiriamali Zuwena Mohamed ‘Shilole’ kuwa Wajumbe wa Baraza la Taifa la Kutokomeza Malaria.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametangaza uteuzi huo leo Aprili 25, 2023 katika Maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani yaliyofanyika Dar es salaam.

“Asilimia 77 ya watanzania ni vijana imempendeza Rais Dkt. Samia kumteua Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz kuwa Mwakilishi wa Vijana katika Baraza la Taifa la Kutokomeza Malaria akiwakilisha Wasanii wa kiume, Diamond ana followers Mil 15.9 kwahiyo akiandika tu ‘Sio kila homa ni Malaria’ inawafikia Watu Mil 15.9 ndani ya sekunde moja”

“Rais amemteua Zuwena Mohamedi Shilole Mwakilishi wa Vijana Wasanii Wanawake kuwa Mjumbe wa Baraza la Taifa la Kutokomeza Malaria.”ameongeza Ummy.

Habari Zifananazo

Back to top button