Rais samia awateua Mwantumu Mahiza, Peter Ilomo

Skauti Mkuu Mwantumu Mahiza

RAIS Samia Suluhu Hassan leo amewateua Skauti Mkuu wa Tanzania Bi Mwantumu Mahiza na Katibu Mkuu Mstaafu Peter Ilomo kuwa Wenyeviti.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imesema Rais Samia amemteua Mwantumu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Uratibu Mashirika yasiyo ya Kiserikali na Ilomo kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

Advertisement