Rais Samia, Dk Mwinyi wachomoza jezi za Simba

JEZI tano za Simba SC zitakazopandishwa na kuzinduliwa kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro zinatakuwa na majina ya viongozi wa Serikali akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Hussein Ally Mwinyi. Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo Iman Kajula amesema.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo mkoani Kilimanjaro, Kajula amesema majina hayo pia yatajumuisha Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson.

Jezi zitakuwa na majina ya viongozi wa serikali mgongoni Rais wa Jamhuri ya Muungano Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Hussein Ally Mwinyi, Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango, Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge, Dk. Tulia Akson na Rais wa Heshima Mohamed Dewji Mo.” Amesema Kajula.

Zoezi la kukipandisha jezi hizo litaanza leo, Ijumaa jezi mpya za timu hiyo zitatambulishwa.

Habari Zifananazo

Back to top button