Rais Samia kaleta heshima
Mwandishi WetuMarch 23, 2023

KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Jangwani Mohamed Fidahusein amesema miaka miwili ya utawala wa Rais Samia suluhu Hassan amejenga mikakati ya kukuza uchumi, uongozi bora na kuwapa heshima wanawake wa Tanzania na Afrika.
Fidahusein, ameyasema hayo katika shina la CCM mtaa wa Chui jijini Dar es Dar es salaam
Amesema, utawala wa Rais Samia kwa kipindi cha miaka miwili akiwa madarakani , amesimamia nidhamu ya kazi serikalini , kukomesha uonevu,uzembe, manyanyaso na kusimamisha uongozi wa haki.

Alisema kutokana na uchapakazi wake ni wazi kiongozi huyo wa kwanza mwanamke nchini, amewaheshimisha na kuwafanya wanawake wa Tanzania na Afrika kujiamini zaidi kifikra ,kujitegemea na kuheshimika.
Aidha, kada huyo ameshauri makundi ya vijana na wanawake kufanya kazi kwa bidii bila kupoteza muda kwani nguvu walizonazo leo zitumike ipasavyo kuwapa manufaa na kuwekeza kwa kesho yao.
Nimevutiwa na utendaji makini wa miaka miwili ya utawala wa Rais Samia, amefanikiwa kujenga mikakati ya kukuza uchumi imara. Najua wapo ambao kwa makusudi wanabeza mafanikio hayo. Uongozi wa Rais wetu utaacha alama isiofutika katika nchi yetu milelele ” Alisema Fidahussein.
Kada huyo pia alisema kama ambavyo mji wa Roma huko Italia haukujengwa kwa siku moja, ndivyo ambavyo uchumi wowote unapoanza kujengeka , matunda yake huwa hayaonekani machoni mwa watu kwa haraka.
Akizungumzia kuhusu utawalabora ,utawala wa sheria na nidhamu serikalini ,alisema mama huyo ana haki ya kuungwa mkono na vyama vyote vya siasa.
Kada huyo alidai Rais Samia ameshatoa msimamo wa serikali yake , kuitangazia dunia akisema anachukizwa na uonevu, uvunjaji sheria pia akizihimiza kwa ngazi nyingine za serikali kulinda haki za binadamu.
“Kwa kipindi cha miaka miwili ya utawala wa Rais Samia kuna uwazi katika uendeshaji wa taasisi za umma watu wengi wanaacha polepole kutozilalamikia Mahakama na Polisi. Taasisi za ukusanyaji mapato nazo hazionei wala kuwasakama wafanyabiashara “Alieleza
Kuhusu kupanda kiwango cha hamasa za michezo hususan mpira wa miguu, Fidahussein alisema katika utawala wa Rais huyo timu za Simba na Yanga zimeanza kuonyesha makali baada ya kufuzu kuingia robo fainali ya michuano ya klabu bingwa Afrika.
“Wakati serikali ya awamu ya sita ikijijenga Kimataifa , Kidiplomasia na kwenye taasisi za fedha .Viongozi na makada wa Chama lazima tuzidi kukiendeleza Chama chetu . Tutapita kila mtaa, nyumba kwa nyumba kuelezea utekelezaji wa ilani ya chama “Alisisitiza kada huyo.



