Rais Samia kusikiliza kero za wananchi

Ni kila mwezi, akimuenzi Mwinyi

KATIKA kumuenzi Hayati Ali Hassan Mwinyi Rais wa pili wa Tanzania, Rais Samia anatarajia kutenga muda wa siku moja kila mwezi kusikiliza kero za wananchi.

Akizungumza leo Machi 5, 2024, Katibu wa  Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi  (CCM) Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda amesema Hayati Rais Mwinyi kipindi akiwa madarakani alikuwa na utaratibu wa kusikiliza kero za wananchi kila mwezi.

Amesema, Rais Samia amekusudia kuanzisha utaratibu huo  ili  kudumisha na kudhihirisha kwa vitendo viongozi kuwasikiliza wananchi,  kumuenzi Hayati Rais Mwinyi aliyekuwa na utaratibu huo na kwa mujibu wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi  na Katiba inayosema tumia cheo chako kwa manufaa ya wengine.

Aidha, amesema mwananchi atakaekwenda kupelekea kero yake kwa Rais lazima taarifa  ya kero zake ziwe hazijapatiwa majibu ngazi ya chini.

“Rais atamsikiliza mtu yeyote bila kujali elimu wala rangi, ndio tumetangaza, hivyo utaratibu utapangwa na wananchi watatangaziwa,” amesema Makonda.

Amesema utaratibu huo utakuwa ukifanyika katika Ofisi ya Chama (CCM), Lumumba Dar es Salaam, Dodoma au Zanzibar kutokana na mahali atakapokuwa Samia ambaye pia ni mwenyekiti wa chama hicho tawala.

Habari Zifananazo

Back to top button