RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema kabla ya kurejea nchini kwa Mwenyekiti wa Chadema, Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema alimtaarifu nia yake hiyo na kumruhusu kurejea pamoja na kufuta kesi zake.
“Mdogo wangu Lema amerudi, aliniambia anataka kurudi nikamwambia rudi, kasema mama nina kesi, nikasema nazifuta rudi.
” amesema Rais Samia akiwa Arusha kwenye ziara yake.
Rais Samia amesema hawachukulii viongozi wa vyama pinzania kama maadui: “Nawachukulia kama watu watakaonionesha changamoto zilizopo nizitekeleze, ili CCM iimarike,” amesema Rais Samia na kuongeza:
“Mwanaume ni yule anayejiamini, mwanamke ni yule anayejiamni, kwa hiyo kwenye uwanja wa siasa tunajiamini, tuko vizuri na tutakwenda vizuri.”