Rais Samia: Limeni zaidi

RAIS wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewahimiza wananchi wa Mkoa wa Manyara  kulima zaidi na kuhifadhi mazao yao na kutahadharisha dunia kukumbwa na bao la nja kwa miaka ijayo.

Akizungumza katika ziara yake Mkoani Manyara leo Novemba 23, 2022 Rais Samia amesema serikali inaendelea kuchukua hatua zaidi katika kukuza kilimo nchini.

Rais Samia Suluhu Hassan akiwahimiza wananchi kulima zaidi

Amesema Mkoa wa Manyara unategemewa zaidi kwa kilimo na msimu wa 2021 umezalisha ziada ya chakula tani 264,819 na kuuzwa nje ya mkoa huo.

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe

“Ongezeni jitihada mzalishe zaidi ya msimu uliopita, serikali tumeanza kujenga  maghala na vihenge ambavyo vinakwenda kuchukua tani nyingi za chakula.” Amesema

Katibu wa  Itikadi na Uenezi CCM, Shaka Hamdu Shaka,

Amesema miaka ijayo dunia itakuwa na hatari ya njaa na kwamba Tanzania haitakuwa na sababu ya kulia njaa.

Amesema serikali imechukua hatua ya kuweka miundombinu ya mbolea, umwagiliaji, kuanza kilimo cha mashamba makubwa ili chakula kiwe kingi cha kuweka akiba na kuuza kwa majirani.

“Tanzania Mungu ametupendelea ardhi, nzuri, maji tunayo, mvua zinanyesha kwa wakati wake la maana ni kkinga maji na kuyahidhi yatumike kwenye kilimo na matumizi mengine,” amesema Rais Samia.

Habari Zifananazo

Back to top button