Rais Samia mgeni rasmi siku ya dawa za kulevya

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho Siku ya Kimataifa ya kupiga vita dawa za kulevya ambayo kitaifa yatafanyika Juni 25 mwaka huu wenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Akizungumza leo Juni 19,2023 jijini Dar es Salaam Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo amesema Mamlaka hiyo inawataarifu watu wote kuwa, Juni 25 kila mwaka, Tanzania huungana na mataifa mengine kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani.

Lengo la siku hiyo ni kuongeza uelewa wa jamii na kuhamasisha Umma kushiriki katika mapambano dhidi ya matumizi na biashara ya dawa za kulevya huku akifafanua maadhimisho haya kwa mwaka huu kitaifa, yatafanyika kuanzia Juni 23 Juni, hadi Juni 25 2023 jijini Arusha

“Maadhimisho haya yataambatana na maonesho ya shughuli mbalimbali za udhibiti zinazofanywa na Mamlaka pamoja na wadau wake katika udhibiti wa dawa za kulevya na utoaji elimu kuhusu tatizo la dawa za kulevya.Mgeni rasmi siku ya kilele Juni 25, 2023 ni Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

“Kauli mbiu ya maadhimisho haya ni “Tuzingatie Utu na Kuboresha Huduma za Kinga na Tiba”. Wananchi wote hususani wakazi wa Arusha na mikoa ya jirani mnakaribishwa kushiriki katika maadhimisho hayo,”amesema Kamishina Jenerali Lyimo.

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
neknoyirze
neknoyirze
3 months ago

 I basically make about $14,000 to $18,000 a month online. It’s enough to comfortably replace my old jobs income, especially considering I only work about 10-13 hours a week from home. I was amazed how easy it was after I tried it copy below web…

HERE ——–>> http://www.join.hiring9.com

Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x