Rais Samia mpongeza Dk Tulia urais IPU

RAIS Samia Suluhu Hassan amempongeza Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU).
–
Raia Samia amesema kuchaguliwa kwake kunaonesha ushuhuda wa kazi kubwa anayoendelea kufanya spika huyo na imani ya wajumbe juu yake na taifa kwa ujumla.
–
“Kuchaguliwa kwako pia ni matokeo ya miaka mingi ya kazi, weledi na kujituma katika utumishi wa umma, mfano bora kwa watoto wa kike katika nchi yetu, Afrika na hata nje ya mipaka ya bara letu.” ameandika Rais Samia kwenye mtandao wa X.