MADAKTARI wa Wauguzi wametakiwa kutovunjika moyo na badala yake wachape kazi kwa kuhudumia vema wagonjwa licha ya changamoto walizonazo.
Hayo yamesemwa na Rais Samia Suluhu leo Novemba 23, 2022 alipotembelea hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Manyara.
Amesema wataalam hao wa afya wamechagua kwa ridhaa zao wenyewe kufanya kazi hiyo ya kuwatibu watu hivyo wasiwe na hofu yoyote zaidi ya kufanya kazi yao.
“Ninawatia moyo mfanye kazi ya kuhudumia wagonjwa bila kujali changamoto mlizonazo kwani watu wanawategemea kupitia sekta hii.”Amesema
Nae, Mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Manyara, Dk Catherine Magari amesema hospitali hiyo ina ukubwa wa ekari 14 na watumishi 272.
Amesema majengo ya hospitali hiyo ya rufaa yamegharimu shilingi bilioni 10.5
“Fedha hizo zimefanikisha ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje, jengo la mama na mtoto, mtambo wa kuzalisha hewa tiba ya oksjeni, jengo la damu salama, majengo ya EMD Radiolojia na wagonjwa mahututuli yaani (ICU),” amesema Dk Magari