RAIS Samia Suluhu Hassan na Rais wa Uganda Yoweri Museveni wamezindua mradi wa kimkakati wa kufua umeme Afrika Mashariki Kikagati – Murongo, Hydropower Plant, Mbarara nchini Uganda
Mradi huo ambao unatokana na maji ya Mto Kagera utakuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 14 na utagharimu dola za Marekani milioni 56.
Akizungumza leo Mei 25, 2023 katika uzinduzi huo uliofanyika katika wilaya ya Isingiro nchini Uganda, Rais Samia amesema umeme utakaozalishwa utaenda kuboresha usafiri na usafirishaji na huduma za kijamii.
“Utaboresha huduma za mawasiliano kati ya miji na vijiji, utaleta usawa katika vijiji na miji kwani umeme utakuwepo kote na pia kuleta muingiliano baina ya watu. Pia utaenda kuboresha ulinzi na usalama.”Amesema Rais Samia
Kwa upande wa Rais wa Uganda, Yoweri Museven amesema ikiwa Tanzania ilitaka MW 2 awali na sasa wanataka 4MW, wapate nne, ninaidhinisha sasa.
“Wakitaka 6MW wanaweza kuchukua, Wakitaka MW 16 zote wanaweza kuchukua lakini wanalipa…..; “ Tunagonjea ndugu zetu Watanzania kutukomboa kutoka kwenye ukosefu wa gesi, sisi huku Uganda tuko na kila kitu hakuna kitu chini ya mbingu tusichokua nacho…lakini gesi yetu haitoshi, tunataka gesi kutengeneza chuma, mbolea na mambo mengine.
Mradi huo ni miongoni mwa miradi inayotekelezwa kupitia uratibu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC.)
Tayari mradi unaofanana na huo umetekelezwa eneo la Rusumo Wilaya ya Ngara ikizinufaisha nchi za Tanzania, Rwanda na Burundi.