Rais Samia mwenyeji mkutano wakuu wa nchi Afrika
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu utakaofanyika jijini Dar es Salaan kuanzia Julai 25- 26, 2023 ukumbi wa mkutano wa Julius Nyerere (JNICC)
Lengo la mkutano huo ni majadiliano ya wakuu wa nchi za Afrika katika kutatua changamoto mbalimbali za ukuaji wa uchumi Afrika kupitia rasilimali watu.
Mkutano huo utajadili uwekezaji kwenye rasimali watu ili kuongeza tija na ajira kwa vijana, kushughulikia maendeleo ya ukuaji wa sekta mbalimbali ikiwemo elimu, nishati na miundombinu kama kichocheo katika kukuza uchumi na kuondoa umasikini.
Ni matarajio yetu kutakuwa na fursa nyingi kwa sekta binafsi Tanzania na kwa nawajasiriamali ambao watafaidika na wageni watakaokuja kwenye mkutano huo kwa kufata fursa ya kuuza bidhaa zao na kutoa huduma mbalimbali.