Rais Samia: Nassari umekua mwanangu

RAIS  Samia Samia Hassan Suluhu amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Monduli,Joshua Nassari na kumwambia sasa amekua.

Rais Samia, ametoa pongezi hizo leo Juni 24, 2023 baada ya Nassari kuongoza sala ya kumwombea na mambo mbali mbali katika nchi eneo la Tengeru wilayani Arumeru akiwa njiani kuelekea jijini Arusha.

“Nakushukuru  Nassari kwa sala, sasa umekua mwanangu, asante sana,mimi si mtu wa maneno mengi wakisema mimi nasonga mbele, nawaahidi vijana serikali itaendelea kufungua fursa za kimaendeleo.”Amesema Rais Samia

Amesema,  serikali bado  inafungua njia kwa ajili ya sekta binafsi na inajipanga vema kuhakikisha vijana wanapata ajira ili kujikwamua kwani anataka kuona vijana wanakuwa na  uchumi imara kwa ustawi wa maisha yao na familia zao na kusisita kuwa kwa vijana wa vyuo serikali itaendelea kuhakikisha vijana wa vyuo vya kati wanapata fursa mbalimbali za mikopo

Aidha, amewaahidi wananchi wa Arumeru la kuhusu ujenzi wa soko la kisasa la Tengeru,Rais Samia amesema serikali inatafuta fedha zaidi kwaajili ya ujenzi wa soko la kisasa la Tengeru.

Habari Zifananazo

4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button